t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Change Tanzania platform and services:


TEGETA ESCROW

Mapitio ya Change Tanzania kwa maazimio ya kamati ya PAC na maoni juu ya hatua zaidi #TEGETA ESCROW Change Tanzania tunatoa shukrani kwa Watanzania wote wanaoendelea kusaini tamko la kutaka uwajibikaji kamili wa serikali na bunge dhidi ya wote waliohusika katika ukwepuaji wa pesa zilizokuwa katika akaunti ya udhamini pale Benki Kuu almaarufu akaunti ya Tegeta Escrow.

Tunawasihi Watanzania wote wenye kutakia mema nchi yetu waendelee kusaini tamko hili https://secure.avaaz.org/en/petition/Wito_kwa_Wabunge_na_Rais_wa_Jamhuri_ya_Muungano_wa_Tanzania

WITO WA KUHAKIKISHA UWAJIBIKAJI KAMILI UNATENDEKA NA PESA ZA /share/? new Bila shaka sote tumeshuhudia juzi Jumamosi tarehe 29/11/2014 kamati ya PAC ikisoma tena maazimio ya bunge yaliyotokana na maridhiano baada ya mkutano wa Bunge wa ijumaa tarehe 28/11/2014 kuvunjika bila mwafaka. Change Tanzania tunapenda kutoa msimamo wetu kuhusu mapendekezo hayo yaliyotokana na mwafaka wa wabunge wa pande mbili yaani upinzani na chama tawala CCM. Tunawapongeza wabunge kwa kupiga hatua kukubaliana juu ya hatua za mwanzo kuelekea uwajibikaji wa viongozi na wahusika katika ukwepuaji wa fedha hizi za umma. Hata hivyo mojawapo ya matakwa ya tamko letu wananchi ilikuwa ni uwajibikaji kamili wa wahusika serikalini. Kutokana na ripoti ya PAC iliyojengwa juu ya ripoti maalum ya ukaguzi wa CAG na ushahidi wa PCCB uhusika wa viongozi wa serikali ni mpana sana katika jambo hili na unatambuka katika wizara zaidi ya moja, ni wazi kuwa Kiongozi wa shughuli za kila siku wa serikali ambaye kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Waziri Mkuu hawezi kuepuka kuwajika. Tulimsikiliza juzi kwa makini katika hotuba yake ya kuahirisha bunge, Waziri Mkuu hata hakuomba radhi kwa Watanzania pamoja na maazimio ya wazi kabisa kwamba viongozi waandamizi katika serikali anayoiongoza walihusika moja kwa moja.

Change Tanzania tunaamini kuwa maridhiano kati ya vyama kuleta mwafaka kati yao ni muhimu kwa taifa letu. Hata hivyo kama taasisi inayotaka kujenga misingi ya mabadiliko katika nchi tunasimamia viwango vya juu vya uwajibikaji kwa wananchi na taifa. Bado tunaamini ili kuondoa dhana ya kuwatoa kafara baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwa makosa ya kimaadili na utendaji ni muhimu kiongozi wao akachukua hatua hii muhimu kuwajibika. Haiingii akilini kwamba Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu Eliakim Maswi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali bw Werema na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Prof Anna Tibaijuka, walitenda shughuli zilizosababisha ukwepuaji huu bila ya Waziri Mkuu kujua walau nini kilikuwa kinaendelea. Isitoshe ufunguaji wa akaunti za dharura katika mabenki, uhamishaji wa pesa taslimu na ugawaji kwa viongozi wa serikali na wa siasa ulifanywa katika mazingira ya kijinai mno, usingeweza kutendeka bila ya vyombo vyetu vya usalama ambavyo tunaviamini kwa ueledi wake mkubwa bila kuwa na habari kabisa. Kuwajibika kwa Waziri Mkuu kutatoa somo kwa viongozi wote ndani ya serikali kwamba wananchi hatutaki lelemama kwa wale waliopewa dhamana ya kutupeleka katika nchi ya maisha bora. Bado tunaamini kuwa mapendekezo ya mwanzo ya PAC yalikuwa ndiyo mwafaka na yaliakisi uhalisia wa makosa yaliyotendwa na viongozi andamizi wa serikali. Tunaamini pia haikuwa sahihi kwa baadhi ya wabunge kuchukua msimamo wa kupinga uchunguzi wa PAC, CAG na PCCB kwa nia ya kuokoa watu wasiozidi 10 kwa gharama ya wananchi zaidi ya milioni 45. Tunaamini Tanzania yetu itabadilika tu pale kila mmoja wetu atakapoamua kubadilika na kwamba viongozi wetu bila kujali itikadi zao za kisiasa wana dhamana kubwa.


Posted on : 14 January, 2019