t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Change Tanzania platform and services:


Mapendekezo Ya Katiba Mpya Baraza La Change Tanzania

Kifuatacho ni ripoti fupi ya mjadala uliofanyika na wanachama wa Change Tanzania katika baraza isiyo rasmi ya katiba tarehe 24 mwezi wa nane, mwaka 2013. Mapendekezo na maoni haya ndiyo yaliyowasilishwa pia katika bunge maalum la katiba kupitia mwakilishi wetu Maria Sarungi-Tsehai, Pia Change Tanzania bado inaendelea kusimamia misingi hii muhimu ya uhuru wa kupata habari na uwajibikaji.

 

MAONI NA MAPENDEKEZO KWENYE KATIBA MPYA. UHURU WA KUPATA HABARI

1.Uhuru wa jambo hilo la kupata hapbari ni muhimu sana katika sehemu mbalimbali za nchi yetu hii ya Tanzania, hivyo tungependa kupendekeza kuwa ibara ya (30 sehemu ndogo ya 4) ni bora ifutwe katika katiba hii, kwa kuwa kuna kifungu cha 29 (2)b tayari imesha eleza juu ya umuhimu wa namna na haki ya kupata habari kama mwananchi na ni haki yake ya msingi.

 

2.Tungependa kuwa ibara ya 30 (4) ni bora iwekwe kwenye sura ambazo zinahusika na usalama wa taifa sura ya 15 kwani inampa fursa na uwanja mpana wa kujadiliwa katika katiba kuliko nafasi ya kujadili ndani ya bunge kwani nafasi ya kujadili ndani ya bunge kwani nafasi yao ni ndogo na hakuna uwanja mpana kuliko katika katiba.

 

3.Kuwepo kwa vyombo vya umma ambavyo havihusiani na vyama vya siasa na view na uhuru wa kutoa habari pasipo kuwa na vikwazo katika katiba za vyama mbalimbali vya siasa.

4.Pia serikali isiingilie uhuru wa habari kwa upande wa bajeti ya vyombo hivyo, tunapendekeza kuwa ni bora bunge liwajibike katika usimamizi wa bajeti zao.

 

5.Mwisho katika hili la habari, tunaomba kuwe na tume huru ya usajili na usimamizi wa vyombo vya habari, ambayo ipendekezwe na uteuzi ufanywe ndani ya bunge.

 

UWAJIBIKAJI WA TAASISI NA VIONGOZI KWA WANANCHI NA KUOANISHA MFUMO WA UWAJIBIKAJI

1.Haki ya ajira kwa vijana katika taratibu za ujira au katika katiba hii mpya ambayo haijafafanua rasmi hujira kwa vijana kwani ajira zinazo tolewa kwa vijana zimewabana sana vijana ususani wanao toka vyuoni yaani wahitimu kwa kutakiwa kuwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 2, kwa hiyo kuna wataka vijana kuwa na uzoefu ni vyema wawaandalie, serikali iwagharamie vijana kwa kuwapa ruzuku ili wapate uzoefu.

 

2.Haki ya wajane: katika rasimu hii haijaonyesha haki za wajane kama haki zingine kwa hiyo kwenye katiba hii tunapendekeza kuwe na haki ya wajane.

 

3.Katiba hii haijafafanua huduma ya watu maalum kama vile walemavu, kwa kupata elimu bora, ulinzi, malazi na tiba.

 

4.Katiba hii inasema Ardhi ni mali ya raisi kwa hiyo tunaomba Ardhi iwe mali ya mwananchi isipokuwa serikali iweke utaratibu mzuri kwa wananchi waweze kugawana Ardhi vizuri kama mali yao.

 

5.Haki ya elimu, rasimu hii ya katiba inasema kila mtu anahaki ya kupata elimu bora, lakini tunaona bado kuna ukandamizaji wa elimu kwa kufuata wenye kipato na kuwabaguwa wasio na kipato kama vile shule binafsi wanasoma watoto wa matajiri tu, kwa hiyo tunaomba rasimu rasimu hii ifafanue kipengele hicho upya.

 

6.Haki ya waliopata ajali, katika rasimu hii haikuongelea kabisa haki ya waliopata ajali na kuwa vilema, hivyo tunapendekeza kuwa wahudumiwe na serikali kwa kuwapa mahitaji mbalimbali.

 

7.Uhuru wa ndoa katika jamii, katika rasimu hii ya katiba, kulingana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971na kufanyiwa marekebisho mwaka 2002 inaweka wazi uhuru wa ndoa, na kwa kutokuwa na mwingiliano kwa wazazi na wanandoa pamoja na koo kwa koo au kabila kwa kabila. Kwa hiyo tunapendekeza kuwa katika katiba ijayo iweke vizuri sheria ya ndoa kwenye katiba mpya.

 

8.Ibara ya 92(4) Neno "Hazitakuwa" ifutwe na Neno "Vitakuwa" liwekwe badala yake.

 

9.Ibara ya 96(3) Mawaziri wawajibike mmoja mmoja bungeni.

 

10.Ibara ya 115(2) kirekebishwe na endapo Bunge litakataa kwa Mara ya pili kwa kura zaidi ya theluthi mbili basi Rais atalazimika kuvunja Baraza la Mawaziri.

 

11.Ibara ya 108(2) kifutwe kwa sababu kinapoka mamlaka ya Bunge ya Kuisimamia na Kuiwajibisha Serikali.

 

12.Ibara ya 113(1) ifutwe kwa sababu inapoka Mamlaka ya Bunge kama yalivyoainishwa kwenye Ibara ya 107(1). m)            Ibara 200(1) Uteuzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ufanywe na Bunge baada ya kupendekezwa na tume ya utimishi ya Bunge.

 

13.Ibara ya 202(4) Kirekebishwe.Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali awasilishe ripoti ya Ukaguzi Bungeni badala ya Rais.Atakapowasilisha Bunge lijadili hiyo ripoti na kutoa mapendekezo na inapohitajika hatua stahiki.

 

14.Ibara ya 202(5) kifutwe.

 

15.Ibara ya 204(5) Mamlaka ya kumwondoa kazini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yawe ya Bunge na si Rais.Hii ni kuimarisha dhana ya Uwajibikaji.

 

16.Rasimu iko kimya kuhusu utaratibu wa kumwondoa Jaji Mkuu kazini.Utaratibu wa kumwondoa Jaji Mkuu madarakani uwe sawa sawa na ule unaotumika katika kumwondoa Rais madarakani.Hii itakazia Uhuru wa mhimili wa Mahakama katika kufanya shughuli zake.

 

17.Bajeti ya Mahakama ikipitishwa na Bunge basi itolewe bila kucheleweshwa au kubadilishwa.Iwe marufuku kwa hazina kubadilisha matumizi ya bajeti ya Mahakama kwa namna yeyote ile;

 

URAIA IKIWA NI PAMOJA NA URAIA MBILI, UPATIKANAJI WA URAIA NA HAKI ZA RAIA WA TANZANIA KWA UJUMLA

A.Katika ibara ya 37 (2) hakuna mamlaka yeyote wala sheria itayotungwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania itakayomuondolea mwanachi uraia wake wa kuzaliwa kwa lazima.

 

B.Kila raia ana haki ya kutambuliwa uraia wakekwa madhumuni hayo bunge liunde sheria, itungwe sheria hii ilikuweka masharti pindi madhara kama haya yakitokea baada ya utaratibu utaowekwa kisheria kufatwa.

 

1.Katiba ijayo iweke wazi kuhusu Uraia uwe wa chi moja tu, uraia ni haki ya binaadamu kila mtu ana haki ya kuishi na kupata mahitaji yote muhimu kama raia katika nchi yake.

 

2.Ibara ya 1 (2) neon Tanzania bara litolewe iandikwe kuwa ni jamhuri ya Tanganyika. wazungumzaji katika Baraza la Katiba la #ChangeTanzania 24/08/2013 Taarifa kuhusu Baraza la Katiba la Change Tanzania https://www.facebook.com/events/622501621114767/ kama ilivyopangwa Tarehe 24/08/2013, Tulikuwa na wazungumzaji wafuatao: John Ulanga - Mkurugenzi mtendaji wa Foundation for Civil Society Dr Azaveli Lwaitama - Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Tumaini na mhadhiri mstaafu wa UDSM Irenei Kiria - Mkurugenzi mtendaji wa SIKIKA Daniel Welwel - mwanasheria wa Mahakama Kuu, na mwanasheria wa Asyla Attorneys pia mwanaharakati Deodatus Balile - Mhariri Mtendaji wa gazeti la JAMHURI From Topics point of view: Ulanga - Utangulizi – Tanzania tuko wapi na mwelekeo wetu kama taifa? Dr Lwaitama na Irenei - Uwajibikaji wa taasisi na viongozi kwa wananchi na kuoanisha mfumo wa uwajibishaji Dan Welwel - Uraia ikiwa ni pamoja na uraia mbili (dual nationality), upatikanaji wa uraia na haki za raia wa Tanzania kwa ujumla Balile - Uhuru wa kutoa na kupata habari


Posted on : 14 January, 2019