t

Update

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Change Tanzania platform and services:


Change Tanzania Yaandaa Mjadala Kuhusu Haki Na Wajibu Wa Raia

20 February 2019, Dar es Salaam: Change Tanzania imeandaa jukwaa la kuwapa wananchi nguvu, hamasa na kujenga bidii ya kushiriki katika maendeleo na kuwa kiungo muhimu kusimamia na kufuatilia masuala mbalimbali ya nchi. Jukwaa hili la kuelimisha wananchi kuhusu la haki na wajibu wa raia limelenga kukutanisha wananchi na wataalamu tofauti kuhusu mada hii. Kaulimbiu ya jukwaa ni “Wenye Nchi ni Wananchi” 

 

Jukwaa linaratibu majadiliano juu ya haki na wajibu wa wananchi  katika katiba na kuhamasisha uanaharakati huru unaoendeleza na kukuza roho ya kujuitolea kusaidia jamii. Jukwaa pia limetoa nafasi ya mjadala mpana zaidi kama vile  mada kuhusu changamoto zinazosababisha kushuka kwa uhuru wa wananchi kujieleza Tanzania pamoja na fursa kwenye uanaharakati wa mtandaoni kama kifaa cha maendeleo kinachoweza kutumika na kila mwananchi. 

 

Akizungumza katika jukwaa hilo, Mratibu wa Taifa wa Change Tanzania, Bw. Mshabaha H. Mshabaha amesema, “Change Tanzania inawahamasisha watanzania wote kuchukua hatua na kuwa na uchu na mwelekeo mzuri wa nchi. Wananchi wana haki ya kuwajibisha watendaji kwa mfano, mwenyekiti wa Serikali ya mtaa, afanye vizuri au mawaziri wanatakiwa wawajibike au wawajibishwe, kwa sababu wananchi ndo waliowapigia kura na kuwapa hiyo kazi ya kuwaongoza. Kikatiba wananchi ndio wamiliki wa nchi, na viongozi ni wawakilishi tu wa wananchi  na wanatakiwa kusimamia matakwa ya wananchi. Pale wananchi wanapotoa hoja mbalimbali au malalamiko wasikilizwe, mijadala ndio afya ya uongozi bora." 

Kwa kuweka kumbukumbu sawa, hili ni jukwaa la pili kuandaliwa na asasi ya  Change Tanzania tangu mwaka 2016. Change Tanzania ni harakati zinazosukuma na kuhamasisha maendeleo kwa kutumia mitandao ya kijamii, na kusimamia uhuru wa kujieleza wa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wananchi kujadili, kukosoa na kutoa taarifa kupitia mitandao.

 

“Kamwe kukosoa sio kukosa uzalendo bali ni kusaidia kujenga misingi imara na uongozi bora, sisi ni kioo, na kazi kubwa ya kioo ni kuonyesha mapungufu ili mapungufu hayo yaweze kurekebishwa na kufanyiwa kazi. Viongozi wanatakiwa kuheshimu na kufuatilia sana maoni ya wananchi. Kwa sasa wananchi wengi wameitelekeza nchi yao kwa viongozi tu kwa matarajio kwamba maendeleo ni lazima yaletwe na viongozi bila ya wao kushiriki kwa hali, mali, maarifa au nguvu kazi.” alieleza Mshabaha H. Mshabaha

 

Change Tanzania imezindua rasmi jukwaa la wito (petition platform). Katika jukwaa hili maoni na matarajio mbalimbali ya wananchi yatachukuliwa na kuwasilishwa kunako stahili. Lengo kubwa likiwa ni wananchi kuisimamia serikali.  Jukwaa la wito la Change Tanzania litakuwa ni daraja kati ya mwananchi na serikali, kupitia jukwaa hili malalamiko au wito utakaoletwa na mwananchi mmoja utapata baraka za wananchi wengine kupitia sahihi ya kidijitali. Wito unapotolewa wananchi wengine watatakiwa kuusoma na kuweka sahihi kama ishara ya kukubaliana na hoja za mtoa wito. Wito utakaowasilishwa unaweza kuwa wa kupongeza au kutaka maboresho ya sheria au kushinikiza upatikanaji wa huduma bora.

Change Tanzania imejenga jukwaa hili mahsusi kabisa ili wananchi waepukane na gharama kubwa ya kuwafuata viongozi kwa ajili ya kuwapelekea maoni yao. Kupitia jukwaa la wito, mwananchi popote alipo anaweza fungua wito Change Tanzania itachukua wito husika na kupeleka kwa mamlaka zinazohusika au kiongozi anayehusika ili kuweza kufanyiwa kazi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na: Mshabaha H. Mshabaha Barua pepe mshabaha@changetanzania.org Simu: 0656064808


Posted on : 27 February, 2019