t

Petition

TERMS AND CONDITIONS

Welcome to our website. If you continue to browse and use this website, you are agreeing to comply with and be bound by the following terms and conditions of use. If you disagree with any part of these terms and conditions, please do not use our website.

The use of this website is subject to the following terms of use:


You may not do any of the following while accessing or using the Change Tanzania platform and services:


WITO KWA SPIKA WA BUNGE KUJIUZULU NAFASI YAKE YA USPIKA #NdugaiJiuzulu #NdugaiMustResign

Posted on : 16 April, 2019

Tarehe 14/04/2019, Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, aliitisha mkutano na waandishi wa habari, pamoja na mambo mengine, akihimiza uamuzi wa Bunge kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Musa Assad, kutokana na kauli ya CAG kwamba Bunge ni dhaifu - hotuba nzima iko hapa.  

Spika amesema kuwa, Bunge haliwezi kushirikiana na CAG na amemshauri CAG kwenda kumuomba msahama Mheshimiwa Rais kwakuwa, kusema Bunge ni dhaifu wakati Mheshimiwa Rais akiwa ni sehemu ya Bunge, ni kulitukana Bunge na Rais pia na kwamba, CAG anampa wakati mgumu Mheshimiwa Rais (Gazeti la Mwananchi limemnuku hapa.)

Hata hivyo, sisi kama wananchi tunaona hatua hii ya Spika si muafaka. Hotuba yake, kwa ujumla, ilibeba mashambulizi dhidi ya CAG badala ya kuangalia mashiko yaliyomo katika Ripoti iliyotolewa na CAG. Spika ameonesha wazi nia na lengo la kuathiri utendaji kazi wa Ofisi ya CAG kwa kuweka shinikizo la CAG kujiuzulu.

Kauli ya Spika imekuja siku chache baada ya CAG kuwasilisha ripoti ya ukaguzi ya mwaka 2017/2018 na kupokelewa Bungeni. Ripoti hiyo imeibua masuala mengi ambayo pasi na shaka, yanaonesha ombwe kubwa katika usimamizi wa fedha za serikali na udhibiti wamatumizi yake. itakumbukwa kwamba, fedha za umma ni fedha zinatokana na jasho letu walipa kodi ambao tunaitwa wanyonge. Hata fedha za marafiki na wahisani wa Taifa letu, zimemaanisha kutumika kwa mujibu wa sheria na kwa malengo kusudiwa.

Katika wakati huu ambapo wananchi katika vikundi, mitaa, makazini vijiweni, katika daladala na mitandao ya kijamii wanajadili Ripoti ya CAG, ni aibu na fedheha kubwa kwa Spika kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kumshambulia CAG, Prof. Assad na kumtaka CAG Prof Assad ajiuzulu.

Katika mamlaka ya Bunge, hakuna mahali Bunge ama Spika wa Bunge amepewa mamlaka ya kuingilia kazi ya CAG, lakini pia, kuna tofauti kati ya kushughulika na masuala yaliyoibuliwa katika Ripoti na kushughulika na mtu binafsi, yaani Prof. Mussa Assad. Kikatiba, Spika hana mamlaka ya kuingilia uteuzi na hata majukumu ya CAG kikatiba.

Moja ya jukumu la Bunge ni kuidhinisha fedha (Bajeti) ambazo ni kodi za wanachi. Jukumu la pili ni kuchambua namna ambavyo fedha hizo zimetumika, jukumu ambalo ni muhimu zaidi kwa Bunge. Hatua ya Spika kumtishia CAG na kumtaka ajiuzulu ni usiginaji wa Katiba. Ni kuingilia uhuru na utendaji wa CAG kwa kumpangia maneno ya kutumia katika kazi zake.

Kwa hatua hii, na kwa sababu zifuatazo; tunamtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndugu Job Yustino Ndugai, ajiuzulu nafasi yake ya Spika, kwakuwa:

1.    Spika ameingilia majukumu ya CAG kwa kumpangia maneno ya kutumia katika kazi yake ambayo ni kinyume na Katiba. Kwa muktadha huu, Spika amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo aliapa kuilinda na kuiheshimu.

2.    Spika Ndugai ameeleza kuwa CAG anampa wakati mgumu Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo ambalo linaweza kumpa hofu CAG na kuathiri utendaji kazi wa CAG.

3.    Spika Ndugai amemtaka Prof Asaad kujiuzulu kwakua Bunge haliwezi kufanya kazi nae, hili ni kosa kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tamzania ya mwaka 1977 ambayo inaelezea vyema kuhusu ukomo wa utendaji wa Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali CAG.

4. Kitendo cha Spika kumshambulia CAG kwa ubinafsi wake ni kinyume na maadili ya utumishi, kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inatoa haki ya mtu kuheshimiwa na kupata hifadhi ya utu wake. Spika amekanyaga Katiba kwa kumshambulia CAG ambaye anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba.

5.    Spika ameonesha nia ya wazi ya kufifisha mjadala wa Ripoti ya CAG wakati ambao tunategemea yeye kama Spika achukue nafasi kuwaongoza wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi katika kujadili Ripoti hiyo.

6.    Kwakuwa ameonesha nia ovu na ya waziwazi ya kukataa kufanya kazi na CAG ambaye ni jicho la wananchi, anakosa uhalali wa kuendelea kuwa kiongozi wa taasisi adhimu inayotegemewa kusherehekea uhuru wa maoni, uwazi, uwajibikaji na utawala wa sheria.

7. Spika Ndugai ameonyesha wazi kuwa kinyume na CAG na yeye akiwa kama kiongozi mkuu wa Bunge inatia shaka utendaji, usimamizi, usawa na uwazi katika uchambuzi wa ripoti ya CAG sisi kama wananchi hatuna imani na utendaji kazi wa Spika kwa sasa.

8.    Spika Ndugai, kama ilivyo kwa viongozi wengine na maspika wengine Duani, alipaswa kuonesha kwa watanzania kuwa Bunge sio dhaifu kwa utendaji na usimamizi imara usio na shaka kwa serikali. Hatua yake kuamua kushughulika na CAG na kuacha kufanyia kazi Ripoti inaondoa imani ya wananchi kwa Bunge. Spika ameonesha hasira ambazo zinaliondoa Bunge katika nafasi yake ya kuwa Chombo cha kuwawakilisha wananchi.

9.    Spika anapaswa kujiuzulu ili kulipa heshima Bunge letu tukufu na kurudisha imani ya wananchi juu ya kazi, majukumu na uimara wa Bunge.

Tunaomba Spika Jobu Ndugai ajiuzulu kwakuwa amekiuka miiko na taratibu za uongozi hivyo sisi wananchi hatuna imani na yeye kusimamia chombo adhimu kama Bunge, ambacho kinatuwakilisha sisi wananchi; kwa ujumla, amepoteza sifa hizo.

#NdugaiJiuzulu #NdugaiMustResign
Reasons for Signing


AdamstenUB AdamstenUBHi savings lover! What can you buy online? Yes, almost everything! So, for everything you can get a significant percentage of cashback from our service! Our regular users know that using a <a href=http://bit.ly/2UwSyfW>cashback service cashback service</a> you can not only profitably buy clothes and equipment, but also save money on purchases of household chemicals, cosmetics and the mass of other categories of goods. And with us you can get a cashback with each order of your favorite food! We are constantly expanding our list of partners among online stores, choosing the most popular of them, so that you don’t have to limit yourself to choosing! Choose from thousands of brands and a million products of various categories! And, of course, get cashback from each order! Visit our website right now and reduce your spending on purchases! Save up to 40% from each purchase !. Use <a href=http://bit.ly/2UwSyfW>cashback service cashback service</a>s. Introducing the largest <a href=http://bit.ly/2UwSyfW>cashback service cashback service</a> in the world! - 2078 popular online cashback stores - 969 stores with increased cashback Today, bank cards are not only a way to store money and non-cash payments, but also a very interesting financial instrument, opening a number of convenient and profitable functions for their owners. Cashback has become a favorite subject in many of the features of related cards. Fast cash withdrawal in a convenient way! http://bit.ly/2VYijaH 4 days ago


Albert busililihatufai kabisa, Mheshimiwa mhimili wa bunge umemshinda. too many drama 1 week ago


Shilla BernardNdugai has failed to rule the parliament democratically, he has failed pstliament rules as enacted. then he must resign. He must go. 2 weeks ago


Bariki AyumwiHis not standing with right 3 weeks ago


olympia MashaloI need my right as a citizen 3 weeks ago


Nganogelwe kimamleameshindwa kuisimamia serikalui 3 weeks ago


Cloud MlaponiMore information 3 weeks ago


piere BashitezeroCag anasimamia haki ukweli na uwazi 3 weeks ago


Mathias KakuruHe must resign 3 weeks ago


2028 have signed. Lets get to 3000

AdamstenUB AdamstenUB signed 4 days ago...

Jose Kitali signed 5 days ago...

Marck Anyimike signed 1 week ago...

Emmanuel Paul signed 1 week ago...

Albert busilili signed 1 week ago...

Dr Julius signed 2 weeks ago...

By signing, you accept Change Tanzania’s Terms of Service and Privacy Policy, and agree to receive occasional emails about campaigns on changetanzania.org. You can unsubscribe at any time

Do You Need Help..?


Join our | WHATSAPP | OR | TELEGRAM | Group for petition updates and actions.
Email: support@changetanzania.org